MICHUZI: Wanaouza pembejeo za ruzuku kwa bei ya juu kuchukuliwa hatua - mkuu wa mkoa wa lindi

MICHUZI
Libeneke la Globu ya Jamii 
thumbnail Wanaouza pembejeo za ruzuku kwa bei ya juu kuchukuliwa hatua - mkuu wa mkoa wa lindi
Jul 27th 2013, 19:23, by noreply@blogger.com (MUHIDIN MICHUZI)

Na Abdulaziz video,lindi

Mkuu wa mkoa wa lindi Ludovick Mwananzila ameuagiza uongozi wa wilaya ya ruangwa kuwachukulia hatua kali watendaji wa chama cha Msingi na ushirika cha Lucheregwa kwa tuhuma za kuuza pembejeo za ruzuku kwa bei ya juu.

Agizo hilo amelitoa katika mkutano wa hadhara baada ya wananchi wa wilaya hiyo kuulalamikia uongozi huo kwa mkuu wamkoa wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mh. Ludovick Mwananzila
Mwananzila alieleza kuwa kitendo hicho cha viongozi hao kuuza pembejeo hizo kwa bei ya juu kinyume na utaratibu uliopangwa na serikali katk ugawaji wa pembejeo za ruzuku ni ujunjaji wa sheria.

Mwananzila alisema ili iwe fundisho kwa wafanyabiashara wengine wenye tabia kama hizo ni lazima viongozi hao wachukuliwe hatua kali za kisheria ambapo alitoa agizo kwa uongozi wa wilaya kuwashughulikia viongozi hao haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wake katibu mkuu wachama cha ushirika cha msingi cha kuuza na kununua mazao Lucheregwa Samora fundi alikiri kuuza pembejeo hizo kwa bei ya juu ambapo alieleza kuwa mfuko mmoja wa salfa aliuza kwa shilingi 16500 badala y ash 15000 kama ilivyoagizwa na serikali.

Fundi alisema uamuzi wa kuuza pembejeo hizo kwa bei hiyo ulitokana na makubaliano ya mkutano mkuu wa chama ukiwa na lengo la kuongeza mapato ya chama kutokana na chama kukosa fedha baada ya kuyumba kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kupitia zao la korosho .

Aidha Mwananzila aliitaka halmashauri ya wilaya ya ruangwa kuhakikisha inahimiza kilimo cha mbogamboga ili kusaidia kuinua kipato cha wakulima kwa kuwapatia vitendea kazi , kuwajengea Uwezo ili waweze kufanya kazi zao ka ufanisi Na Kipato ikiwemo Halmashauri hiyo kupata Ushuru.

"""wakulima ili muweze kufanikiwa ni lazima mjiunge kwa vikundi na kuunda saccosz itakazo wafanya muweze kutambulika na taasisi za fedha na kukopesheka'''' Alimalizia Mwananzila.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions
Previous
Next Post »