MICHUZI: MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL APOKEA MAANDAMANO YA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA VIKUNDI VYA MTANDAO WA WAKULIMA WA TANZANIA (MVUWATA) MJINI MOROGORO

MICHUZI
Libeneke la Globu ya Jamii 
thumbnail MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL APOKEA MAANDAMANO YA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA VIKUNDI VYA MTANDAO WA WAKULIMA WA TANZANIA (MVUWATA) MJINI MOROGORO
Jul 26th 2013, 22:24, by noreply@blogger.com (MUHIDIN MICHUZI)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti, mmoja kati ya wachangiaji bora wa kuendeleza Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) Justice Shekilango, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika leo Julai 26, 2013 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wasanii wa kikundi cha ngoma ya Muhembe cha mjini Dodoma, wakitoa burudani wakati wa sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro.
Wakulima wa Jumuiya ya Mtandao wa Wakulima wa Tanzania (MVUWATA) wakiwasili kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa maandamano leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo, yaliyopokelewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, aliyekuwa mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanamtandao wa Jumuiya ya wakulima wa Tanzania (MVUWATA) baada ya kupokea rasmi maandamano ya wakulima ya maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro. Picha na OMR.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions
Previous
Next Post »