DJ Fetty: Picha: Mmiliki wa Home Shopping Center akiwa South Africa kwa matibabu baada ya kumwagiwa tindikali

DJ Fetty
 
thumbnail Picha: Mmiliki wa Home Shopping Center akiwa South Africa kwa matibabu baada ya kumwagiwa tindikali
Jul 25th 2013, 14:00, by noreply@blogger.com (djfatty)


MFANYABIASHARA maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center(HSC), Said Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko  Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Hali yake inadaiwa kuendelea vizuri, lakini kuna uwezekano wa jicho lake moja kutokuona kabisa baada ya kuathirika sana, lakini jicho la pili liko salama.
Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka.

Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki.

Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua.

Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni.

Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani kwake.
its more about music industry and social issues in and out of bongo land

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions
Previous
Next Post »